Bill Gates awasili Kenya kwa ajili ya  ziara yake

Bill Gates awasili Kenya kwa ajili ya ziara yake

Bilionea mkubwa duniani na mfanyabiashara wa Marekani Bill Gates yuko nchini Kenya ambapo anatarajiwa kufanya mazungumzo na Wakenya kuhusiana na masuala mbalimbali.

Mwanzilishi huyo wa Microsoft anatazamiwa kukutana na maafisa wa serikali na washika dau wengine katika sekta ya kibinafsi. Gates atazuru kaunti ya Makueni ambapo mwenyeji wake atakuwa Gavana Mutula Kilonzo Jnr.

Ripoti zinaonyesha kuwa atatembelea hospitali ya Mama na Mtoto ya Makueni na kituo cha afya cha Kathonzweni. Pia atatembelea viongozi wa kitaifa na mitaa, washirika na wafadhili na pia kukutana na wanasayansi wa kikanda na wavumbuzi.

Chanzo BBC


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post