Beyonce aziteka tuzo za Grammy

Beyonce aziteka tuzo za Grammy

Mwanamuziki anayeupiga mwingi kwenye matamasha yake ya kila mwaka, Beyonce ameweka historia nyingine na kuziteka tuzo za Grammy kwa kuteuliwa katika vipengele vingi zaidi, akimpiku masanii wa Pop aliyetawala tuzo hizo mwaka 2024, Taylor Swiff.

Beyonce ameteuliwa kuwania tuzo hizo kubwa duniani katika vipengele 11 huku akipata uteuzi katika vipengele vya muziki wa Country na American Roots kwa mara ya kwanza.

Vipengele hivyo ni pamoja na Wimbo wa Mwaka, Albamu ya Mwaka ‘Cowboy Carter’, Albamu Bora ya Country, Wimbo Bora wa Country, Rekodi bora ya Mwaka kwa nyimbo ya “Texas Hold 'Em” na vinginevyo.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali zinaeleza kuwa ikiwa Beyoncé atashinda tuzo ya albamu ya Mwaka, atakuwa mwanamke mweusi wa kwanza kushinda tuzo hii katika karne ya 21.

Mara ya mwisho mwanamke Mweusi kushinda tuzo hii ilikuwa mwaka 1999 ambapo tuzo hiyo ilichukuliwa na Lauryn Hill kupitia albamu ya ‘The Miseducation of Lauryn Hill’. Huku anawake wengine weusi waliowahi kunyakuwa tuzizo ni pamoja na Natalie Cole na Whitney Houston.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags