Baada Ya Muda Mrefu, Rihanna Aingia Studio

Baada Ya Muda Mrefu, Rihanna Aingia Studio

Baada ya ukimya wa muda mrefu, mwanamuziki kutoka visiwa vya Barbados, Rihanna anatarajia kuachia wimbo mpya Ijumaa Mei 16,2025.

Kwa mujibu wa tovuti ya Billboard, Rihanna ataachia wimbo huo uitwao “Friend of Mine” kwa ajili ya filamu ya Smurfs.

Katika filamu hiyo, Rihanna atacheza sauti ya Smurfette, akishirikiana na waigizaji wengine kama John Goodman, James Corden, Nick Offerman, Sandra Oh na wengineo.

“Friend of Mine” utakuwa wimbo wa kwanza wa Rihanna tangu alipoachia “Lift Me Up” mwaka 2022 ambao ulisikika katika filamu ya Black Panther: Wakanda Forever. Huku akiwa hajatoa albamu yoyote tangu ‘Anti’ ya mwaka 2016, ambayo ilishika nafasi ya kwanza kwenye chati ya Billboard 200 kwa wiki mbili mfululizo.

Licha ya mashabiki kusubiri album na wimbo mpya kutoka kwa msanii huyo kwa miaka tisa lakini Rihanna ameeleza kuwa ujauzito wake wasasa hamzuii kuendelea kufanya kazi zake za muziki

“Ujauzito wangu hauwezi kuchelewesha kazi mpya za muziki, Labda video chache! Bado naweza kuimba,” alisema Rihanna alipokuwa kwenye mahojiano na Entertainment Tonight kwenye zuria jekundu la Met Gala la mwaka huu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags