Aziz Ki humwambii kitu kuhusu mpira wa kikapu

Aziz Ki humwambii kitu kuhusu mpira wa kikapu

Mchezaji wa ‘klabu’ ya Yanga Aziz Ki siku ya jana Mei 29, 2024 alitembelea klabu ya mpira wa kikapu ya Dar City Basketball na kufanya nao mazoezi huku akiweka wazi kuwa mchezo huo ndiyo anaoukubali zaidi.

Mfungaji bora wa msimu wa 2023/24 Ligi kuu Tanzania Bara, Aziz Ki alifunguka machache akieleza kuwa mpira wa kikapu ndiyo mchezo wake wa kwanza anaoupenda zaidi kuliko mpira wa miguu.

Aidha Rais wa timu ya ‘Dar City Basketball’ Mussa Mzenji alipata wasaa wa kuongea na kueleza kuwa Dar City na Yanga wamekuwa na uhusiano mzuri kwa muda mrefu ndiyo maana ilikuwa ni rahisi Ki kufika mazoezini hapo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags