Asake ataja sababu Davido kutokuwepo kwenye album yake

Asake ataja sababu Davido kutokuwepo kwenye album yake

Msanii wa Asake amefunguka sababu ya Davido kutokuwepo kwenye Album yake aliyoipa jina la ‘Lungu Boy’ inayotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Wakati yupo live kwenye Instagram yake Asake alijibu swali la shabiki aliyekuwa akiuliza kuwa kwanini mkali wa Afrobeat Davido hakuwepo kwenye album hiyo kwa kueleza kuwa hajamuhusisha kwenye album hiyo kutokana na wawili hao kuwa na ‘kolabo’ nyingi ambazo hazijatoka.

“Mimi na Davido tuna ‘kolabo’ lakini muda huu ni wa album ya ‘Lungu Boy’ endapo muda ungekuwepo basi na yeye angehusishwa pia”

Licha ya kuweka wazi suala hilo Asake aliwataka mashabiki waelekeze nguvu zao katika album yake hiyo kwani kuna muda atatoa ‘kolabo’ alizofanya na wasanii mbalimbali.

Utakumbuka kuwa Asake alikuwepo kwenye album ya Davido iitwayo ‘Timeless’ kupitia wimbo wao wa ‘No Competition’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags