Argentina yafikiria kuweka sura ya Messi kwenye noti

Argentina yafikiria kuweka sura ya Messi kwenye noti

Maafisa usimamizi wa fedha Argentina inafikiria kuweka sura ya mshambuliaji Lionel Messi kwenye noti za nchi hiyo baada ya mshindi huyo mara 7 wa Ballon d'or kuiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa kombe la Dunia 2022.

Kwa mujibu wa gazeti la El Financiero, maafisa wa bodi ya usimamizi wa fedha nchini humo wanatafuta njia za kuuenzi ushindi wa kihistoria wa Kombe la Dunia wa Taifa hilo nchini Qatar.

Kuweka picha yenye sura ya Messi akiwa na kombe la Dunia kwenye noti za nchi hiyo inatajwa kuwa chaguo bora zaidi kwani tarakimu huanza na '10' ambayo ni namba ya jezi inayovaliwa na GOAT huyo.

Nyuma ya noti hiyo imependekezwa kuwa 'La Scaloneta' ambalo ni jina la utani la kocha wa Argentina Lionel Scaloni.

Hii itakuwa na lengo la kuheshimu mafanikio ya kocha huyo aliyeiongoza timu ya Taifa hilo kushinda Copa America 2021, Finalissima dhidi ya mabingwa wa Euros Italia na ushindi wa kombe la Dunia 2022 dhidi ya Ufaransa Nchini Qatar.

Benki Kuu ya Argentina ilianzisha sarafu za kibiashara kuadhimisha ushindi wa kwanza wa Kombe la Dunia mnamo mwaka wa 1978.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags