Anjella: Harmonize hajanitafuta toka nichore tattoo ya jina lake

Anjella: Harmonize hajanitafuta toka nichore tattoo ya jina lake

Msanii wa muziki wa bongo fleva Anjella amefunguka na kusema kuwa toka achore tattoo ya jina la aliyekuwa boss wake Harmonize, bado hawajawasiliana kabisa licha ya staa huyo kuona alichokifanya na kurepost kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Akiwa katika mahojiano na  moja ya chombo cha habari, mwanadada huyo amesema sababu kubwa kuchora jina la Konde Boy ni kwa sababu ni mtu aliyemfungulia milango na kutambulika kwa watu, hivyo anakumbuka alichomfanyia.


“Nimeona tu amerepost kwenye instagram yake lakini bado hatujaongea chochote na wala bado sikuzungumza nae,” amesema Anjella.


Aidha mbali na hivyo anasema kuwa asilimia kubwa ya watu walioongea nae wamempongeza kwa kitu alichokifanya kwani wanasema amefanya jambo lenye kumbukumbu.

Lakini pia amegoma kabisa kuzungumzia kuhusu kuwa na maelewano mazuri na staa huyo na kusema kuwa kuna siku atayamwaga yote hazarani ila hakimiliki zake anazo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post