Anayedai kubakwa na CR7 aibuka tena mahakamani

Anayedai kubakwa na CR7 aibuka tena mahakamani

Mwalimu na mwanamitindo kutoka nchini Marekani Kathryn Mayorga, aliyedai kubakwa na nguli wa ‘soka’ Cristiano Ronaldo amerudisha kesi hiyo tena mahakamani kwa lengo la kutaka mchezaji huyo wa ‘klabu’ ya Al Nassr kumlipa mamilioni ya pesa.

Kathryn Mayorga alidai kuwa nyota huyo alimshambulia na kumnyanyasa kingono katika chumba cha hoteli huko Las Vegas miaka 15 iliyopita, licha ya Ronaldo kusisitiza kuwa walifanya tendo hilo la ndoa kwa makubaliano na wala hakukuwa na vitisho.

Mwanamitindo huyo inaelezwa kuwa mwaka 2010 walifanya makubaliano ya siri na kulipwa Pauni 275,000, huku Juni mwaka jana Mayorga alirudisha kesi hiyo ya kumshinikiza CR7 kumlipa mamilioni ya pesa, ilifutiliwa mbali na Jaji Jennifer Dorsey baada ya kugundulika alipokea pesa.

Lakini sasa mwanamitindo huyo amewaomba mawakili kuomba rufaa na kufufua tena kesi ya kutaka mamilioni ya pesa kwa mchezaji huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags