Afariki akiwa anamkimbiza mumewe na mchepuko

Afariki akiwa anamkimbiza mumewe na mchepuko

Mmmmmmmmh! Yaani sio pouwa kabisa, kila siku mambo yanazidi kutaradadi bwana weeeh! Kama kawaida yetu sisi kila siku tunakusogezea taarifa mbalimbali zitakazokuelimisha, kuburudisha na zakushangaza zaidi.

Basi bwana Kutoka nchini Nigeria, mwanamke mmoja amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari wakati akimfukuzia mume wake ambae alikuwa kwenye gari lingine na mwanamke ambae inasadikika kuwa ni mchepuko wake.


Aidha, inadaiwa mwanamke huyo alimuona mume wake na mwanamke huyo wakitoka saluni ya kike na kupanda gari la mwanaume huyo ndipo akaamua kuwafukuzia ili aliwahi gari la mume wake kwa mbele ndipo akapata ajali ambayo ilimsababishia umauti.

Mwanaume huyo alivyoona mke wake amepata ajali, alimshusha mchepuko yule kisha kuwahi kumsaidia mke wake ambapo walimfikisha hospitalini lakini baada ya muda taarifa zilitoka kuwa mwanamke huyo amefariki dunia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags