Adele ahifadhi bigijii iliyotemwa na Celine Dion 2019

Adele ahifadhi bigijii iliyotemwa na Celine Dion 2019

Thamani ya kitu hutokana na mtu anavyokichukulia, na wakati mwingine hata mbabe huwa na mbabe wake.

Ikiwa leo ni Jumatano siku ambayo ulimwengu huadhimisha siku ya wanawake waliofanya makubwa kwenye sekta mbalimbali, upande wa burudani tunamuangaza mwimbaji wa Uingereza, Adele ambaye licha ya kuwa mbabe kwenye muziki anaonekana kuvutiwa zaidi na mwanamuziki Céline Dion hadi kufikia hatua ya kuhifadhi kipande cha bigijii kilichotemwa na msanii huyo.

Kipande hicho ambacho Adele amekihifadhi kwenye nyumba yake iliyoko California, Céline alikitema mwaka 2019, aliposhiriki kipindi cha "Carpool Karaoke" kilichokuwa kinaongozwa na James Corden. Ndipo muongozaji alimuomba ateme bigijii iliyokuwa mdomoni na kuiweka kwenye karatasi kisha kuitumia kama zawadi kwa Adele ambaye mara zote alikuwa akizungumzia kuvutiwa na Celine.

Hivyo basi ombi hilo halikuwa gumu kwa Celine. Bigijii hiyo ilitolewa kama zawadi maalum na kukabidhiwa Adele ikiwa ni sehemu ya kujenga urafiki baina ya wasanii hawa wawili.

Katika kuthamini zawadi hiyo Adele, ambaye anajulikana kwa sauti yake ya kipekee mwaka 2021 akiwa kwenye mahojiano na BBC Radio 1 alikiri kwamba anahifadhi kipande hicho cha bigijii kama zawadi ya thamani. Alisema ni kitu cha kipekee cha kukumbukwa kwa sababu kilitoka kwa mwimbaji wa hadhi ya juu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags