6 wauliwa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi wa zamani

6 wauliwa kwa kupigwa risasi na mwanafunzi wa zamani

Watu sita wauliwa, watatu wakiwa watoto na watatu wakiwa ni wafanyakazi kwa kupigwa risasi na mwanafunzi wa zamani katika shule moja katika mji wa Nashville, Marekani.

Watatu kati ya waathiriwa walikuwa wanafunzi wa umri wa miaka tisa.  Polisi waliwataja kuwa ni Evelyn Dieckhaus, Hallie Scruggs na William Kinney, huku watu wazima waliouawa ni Cynthia Peak, 61, Katherine Koonce, 60, na Mike Hill, 61.

Peak alikuwa mwalimu mbadala akifanya kazi shuleni siku hiyo, Hill alikuwa mlinzi na Koonce alielezwa kuwa mkuu wa shule kwenye tovuti ya Covenant.

Aidha, polisi nchini humo walisema mshukiwa huyo alitambulika kwa jina la Audrey Hale mwenye umri wa miaka 28, ambaye alitambuliwa kama mtu aliyebadili jinsia, hata hivyo alidhibitiwa na polisi kwa kupigwa risasi na kufa hapo hapo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags