50 Cent: Nimefanya makosa kadhaa lakini siyo kuoa

50 Cent: Nimefanya makosa kadhaa lakini siyo kuoa

Mwanamuziki wa Marekani 50 Cent amefunguka kuhusiana na suala lake la useja (kuwa single) huku akiweka wazi kuwa amefanya makosa mengi sana lakini hajafikiria kufanya kosa la kuoa.

50 ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye mahojiano na ‘The Late Show With’ baada ya kuulizwa swali na mwandishi Stephen Colbert kama amewahi kuoa ndipo akajibu hatokuja kufanya kosa hilo kwani anaamini kuoa ni kufanya kosa kubwa.

“Hapana, hapana. Niko salama, mimi si mateka mwenye furaha, niko hapa, mwanangu niko huru nimefanya makosa kadhaa, lakini siyo kufanya kosa la kuoa" amesema 50 Cent

Mbali na hayo amedai kuwa kwa sasa ni mseja na amelifanikisha hilo kwa kujizuia na kufanya mazoezi ya kujizuia kutamani au kumfuatilia mwanamke yeyote yule, hivyo basi kwa sasa ataishi bila kufanya tendo la ndoa.

Utakumbuka kuwa Januari mwaka huu 50 Cent aliandika malengo yake ya mwaka huu kupitia ukurasa wake wa Instagram moja wapo likiwa ni la kuwa mseja.

50 Cent amewahi kuingia kwenye mahusiano na wanawake maarufu kama msanii Ciara na mchekeshaji Chelsea Handler lakini pia hivi karibuni amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na mwanamitindo Jamira "Cuban Link" Haines, ingawa haijulikani kama bado wako pamoja.

Hata hivyo ana mtoto wa kiume Marquise Jackson, aliyezaa na Shaniqua Tompkins mwingine aitwaye Sire Jackson, amempata na aliyekuwa mpenzi wake Daphne Joy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags