Wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake mwaka 1983 kupitia ‘Rolling Stone’ alifunguka kuwa anapenda sana kutazama katuni kwani zinamfanya afikirie mambo ya kufikirika ambayo yangemsaidia katika Sanaa yake.

“Mimi ni mkusanyaji wa katuni, Ninazipenda sana katuni. Hizo ndizo ninazopenda. Nazitazama kila wakati, Paul McCartney ndiye mtu pekee ninayemjua mwenye mkusanyo mkubwa wa katuni kunishinda. Ninapomtembelea nyumbani kwake, tunatazama katuni kila wakati.
Napenda kuzitazama kwa sababu unaniruhusu kuwa katika ulimwengu wa kufikirika ambao unanisaidia zaidi katika kazi zangu za Sanaa,” alisema marehemu MJ
Mbali na kueleza mapenzi hayo lakini pia msanii huyo anatajwa kujihusisha katika uchoraji wa katuni mbalimbali zikiwemo za Disney, Looney Tunes, na MGM.
Aidha michoro aliyoichora MJ bado ipo na inamilikiwa na familia yake huku baadhi ya kazi zake zikionyeshwa kwenye maonyesho maalum ya sanaa, na nyingine zikibaki katika mkusanyo wa mali yake (Michael Jackson Estate). Pia, baadhi ya michoro yake iliuzwa kwenye minada kwa mashabiki na wakusanyaji wa sanaa.
MJ alifariki 25 Juni 2009 kutokana na mshtuko wa moyo uliosababishwa na overdose ya dawa ya usingizi iitwayo Propofol.
Daktari wake binafsi, Conrad Murray, alikuwa akimpa dawa hiyo kusaidia Jackson kulala, lakini matumizi mabaya ya dawa hiyo yalileta matatizo ya kiafya na hatimaye kusababisha kifo chake. Baada ya uchunguzi, Murray alihukumiwa kwa uuaji usio wa kukusudia (involuntary manslaughter) mwaka 2011 na alihukumiwa kifungo cha miaka minne jela, ingawa aliachiliwa baada ya miaka miwili.
Leave a Reply