50 Cent kuandaa filamu ya maisha ya Hushpuppi

50 Cent kuandaa filamu ya maisha ya Hushpuppi

Msanii maarufu wa muziki wa rap wa Marekani 50 Cent ametangaza kuwa anatengeneza msururu wa vipindi vya televisheni (series) kuhusu maisha ya mfungwa - Mnigeria na tapeli wa mitandaoni, Hushpuppi.

Tangazo hilo la 50 Cent limezua mjadala mtandaoni huku baadhi wakiunga mkono wazo hilo, huku wengine wakisema utawafanya Wanigeria waonekana vibaya.

Hushpuppi alikuwa maarufu kwenye mtandao wa Instagram ambao aliutumia kuonyesha utajiri wake mkubwa kwa wafuasi wake milioni 2.8, hadi alipokamatwa mjini Dubai mwaka 2020, na akaunti yake kufungwa.

Kutengeneza msururu wa vipindi kuhusu maisha ya tapeli huyo kwa 50 Cent si jambo geni kwani tayari ameshatayarisha filamu kadhaa zilizo fanya vizuri duniani kama vile “Power” iliyoangazia wauzaji wa dawa za kulevya Marekani.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post