50 Cent adai haki ya malezi ya mtoto wake

50 Cent adai haki ya malezi ya mtoto wake

Baada ya ‘rapa’ 50 Cent kugundua kuwa mzazi mwenziye Daphne Joy kuwa alikuwa akilipwa pesa kwa ajili ya kutoa huduma za kingono kwa Diddy, 50 ameripotiwa kudai haki ya malezi ya muda wote ya mtoto wake wa kiume aitwaye ‘Sire’.

Kwa mujibu wa tovuti ya #UsWeekly imeweka wazi kuwa 50 amefanya uamuzi huo wa ghafla baada ya aliyekuwa mpenzi wake Daphne kutajwa katika kesi iliyowasilishwa na Rodney "Lil Rod" Jones dhidi ya Diddy, ambapo mwadada huyo alishutumiwa kuwa mfanyakazi wa ngono wa Diddy.

Aidha kupitia ukurasa wa Instagram wa Cent alieeleza kuwa hakuwahi kujua kama Baby Mama wake hiyo alikuwa ni mfanyakazi wa ngono ‘Sex Worker’ huku akimtaka wakutane katika mahakama ya familia kwa ajili ya kesi ya malezi ya mtoto wake huyo.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post