Shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria limesema watu 14 wamefariki dunia baada ya shambulizi kufanywa katika msafara wa kijeshi wa waasi wanaoungwa mkono na Iran mashariki mwa Syria karibu na mpaka wa Irak usiku wa kuamkia leo.
Shirika la Syrian Observatory for Human Rights lililo na makao yake nchini Uingereza limesema shambulizi hilo limefanywa katika malori yaliyokuwa yamebeba mafuta na silaha katika eneo la mpakani la Albu Kamal. Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani umewaambia waandishi wa habari kwamba hauhusiki na shambulizi hilo.
Afisa mmoja wa ulinzi wa Irak amesema malori hayo yalikuwa yanasafirisha mafuta kutoka Iran kuelekea Lebanon kupitia Irak na Syria. Afisa huyo amesema msafara huo ulijumuisha malori 22 ambapo 10 yalishambuliwa baada ya kuingia Syria.
Leave a Reply