Zijue dalili za mtu mwenye lishe duni

Zijue dalili za mtu mwenye lishe duni

Jamani eeeeeee!!!!!! mwenzenu mimi napenda sana kula, tena chakula kizuri kilichoenda shule watoto wa mjini tunasema.

Hata wewe kijana mwenzangu uliopo chuoni najua unapenda kula tena kuna wakati unawatambia mwenzako kwa kuwaambia kuwa mwili haujengwi na matofali si ndio.

Pamoja na watu kula chakula ila wapo baadhi ambao wamekuwa wakijali sana kazi zao za kila siku na kusahau kabisa kujali afya zao.

Matokeo ya jambo hili husababisha ongezeko la watu wanaopata magonjwa yasiyoambukiza huku wengine kufa vifo vya ghafla.

Suala la kula pengine ndio nguzo ya kwanza muhimu ya afya ya binadamu hivyo mwili ukiwa sawia bila shaka utaweza kufanya mambo yako yote.

Kama mwili hautakuwa sawia hutoweza kutimiza lengo lako lolote ulilojiwekea katika maisha yako.

Hivyo basi leo katika makala tumeamua kukuletea dalili za mtu mwenye lishe duni na Ofisa Lishe, Mtafiti, Elimu na Mafunzo ya lishe kutoka Taasisi ya Tiba na Lishe, Walbert Mgeni anatujuza zaidi.

Anasema dalili ya kwanza ya mtu mwenye lishe duni ni kutokuwa na hamu ya kula ambapo wakati wote hujiona ameshiba na haitaji kupata chakula ili kujenga mwili.

Mgeni anasema mtu mwenye lishe duni hupungua uzito wa mwili hali ambayo inaweza kumsababishia kifo pindi anaposhambuliwa na magonjwa ya kuambukiza.

“Kuna uzito fulani mtu akiwa nao unaweza kumsababishia kifo na ndio maana madaktari wanasema kuwa uzito ukiwa mkubwa sana unaathari na ukipungua sana unaathari zake pia tena kubwa,” anasema

Anasema mtu yeyote mwenye lishe duni ni rahisi kupata magonjwa yanayoambukiza kwani kinga zake za mwili zinashindwa kupambana na chochote.

“Ila mtu akiwa na lishe nzuri anakuwa na kinga imara katika mwili, anakuwa na uwezo mdogo wa kupata maambukizi, lakini akiumwa hupata madhara madogo sana,”anasema

Hivi ndivyo vyakula vyenye kujenga kinga ya mwili

Mgeni anasema ili mwili wa binadamu uwe na afya njema basi hana budi kuhakikisha kila siku anakula vyakula vyenye kujenga kinga ya mwili.

Anasema mtu akiwa na kinga nzuri husaidia mwili kuzuia au kupambana na maambukizi na kuongeza kuwa mfumo mzuri wa kinga unaweza kugundua kwa wakati virusi, bakteria, au vijidudu vingine visivyofaa vinavyovamia mwilini.

Hata hivyo Mgeni anasema vyakula vinavyosaidia kujenga kinga ya mwili vimegawanyika katika makundi matano, ambapo moja ni nafaka, mizizi na ndizi.

“Kundi hili la vyakula vya nafaka, mizizi na ndizi linatoa kirutubisho cha wanga. Kazi ya vyakula hivi ni kuupatia mwili nguvu ambayo itamuwezesha mtu kuweza kutembea, kufikiri na kufanya maamuzi mbalimbali katika maisha yake,” anasema.

Vilevile anasema kundi lingine ni vyakula vyenye asili ya mikunde na wanyama ambavyo hutoa virutubisho vya protini au amirojo huku kazi yake kubwa ni kuujenga mwili.

“Mfano wa mikunde ni maharage, njegere, choroko huku vyakula vya asili ya nyama ya kuku, samaki, ng’ombe na mazao yake ambao ni mayai, maziwa, jibini pamoja na siagi,” anasema

Hata hivyo Mgeni anasisitiza kuwa jamii inapaswa kujiepusha na ulaji wa nyama nyekundu kwani zina athari kubwa katika mwili wa binadamu.

“Nyama ambazo sisi wataalamu wa afya tunawashauri Watanzania kula ni zile nyeupe nikimaanisha kuku, samaki na jamii ya ndege, tuachane na nyama hizi ya mbuzi na ng’ombe kwa kuwa sio nzuri kula mara kwa mara,” anasema

Vilevile anasema kundi linalofuata ni la mbogamboga lakini katika jamii hupenda kuita mboga za majani ambazo huleta virutubisho vya vitamin na madini katika mwili.

“Katika kundi hili tunapata vitamini na madini ambayo ni muhimu kwenye kuukinga mwili dhidi ya magonjwa na kuufanya kuwa na afya njema,” anasema.

Mgeni anaongeza na kusema kuwa karoti, biringanya na bamia vyote hivyo vipo katika kundi la mbogamboga.

“Jamii nyingi hasa za wafugaji na wavuvi zinachukulia kuwa mtu anayekula mbogamboga kama mchicha, matembele, spinachi, mchunga, mnavu ni maskini nawaambia ndugu zangu kuwa mnajidanganya kwani vitu hivyo vinasaidia sana kuboresha kinga ya mwili,” anasema

Mgeni anasema kundi lingine la vyakula vya kujenga kinga ya mwili ni matunda ambayo yana virutubisho aina ya vitamin na madini na kazi yake ni ile ile ya kuisaidia mwili kutopata maradhi.

“Matunda kila mtu anayajua ila Ukwaju upo katika kundi la matunda na una Vitamin C ambavyo ni muhimu sana katika kupambana na magonjwa, wakati wa Corona watu walitumia tunda aina ya ndimu ni kwa sababu lina Vitamin C ambavyo hukinga mwili dhidi ya magonjwa,” anasema

Anasema jamii nyingi ilikuwa ikiamini kuwa ndimu na limao vinakausha damu lakini kupitia ugonjwa wa Corona walibaini kuwa jambo hilo si la kweli.

“Hata hivyo bado kuna shida sana katika kundi hili kwani watu wengi hawana utamaduni kabisa wa kula matunda, sisi tunashauri kama matunda ni bei basi wale kulingana na msimu ili kuepuka kununua kwa bei ya juu,” anasema

Akiendelea kutoa elimu Mgeni anasema kundi la mwisho la chakula kinachojenga kinga ya mwili ni mafuta, sukari na asali

“Kundi hili huzalisha nishati kwa wingi hivyo kuupatia mwili nguvu, ila sasa tunapaswa kujua utumiaji wa vitu hivyi vinapaswa kuwa kwa kiasi maana kama utakula sana sukari, mafuta au asali kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka uzito ambao ukiwa mkubwa una athari katika mwili ikiwamo kupata magonjwa yasioambukiza,” anasema na kuongeza.

"Ukipenda kula keki, sukari, unaweza kupata magonjwa yasioambukza ikiwamo ya moyo, shindikizo la juu la damu, kisukari na mengine, ili kuepuka kuyapata huna budi kutumia vitu hivyo kwa kiasi,”

Mgeni alishauri kuwa mafuta ambao watu wanapaswa kuyatumia ni yale yanayokana na asili ya mmea ambayo ni alizeti, karanga pamoja na ufuta lakini sio mafuta yanayotokana na wanyama.

Anasema pamoja na yote hayo ulaji unaoshauriwa ni ule wa mlo kamili “ukinywa cha asubuhi, ukila chakula cha machana ua usiku hakikisha unakula mlo kamili,”

Hata hivyo Mgeni anasema virutubisho vinavyohitajika kwa wingi mwilini ni protini, wanga pamoja na mafuta huku vinavyohitajika kwa kiasi kidogo ikiwa ni vitamin na madini ambayo yapo ya aina nyingi na husaidia kupambana na maradhi.

Umuhimu wa lishe bora

Mgeni anasisitiza kuwa lishe ni mchakato mzima wa chakula kuanzia kinavyoliwa, kusagwa mwilini na kusisitiza kuwa mtu anavyokula hupata virutubisho mbalimbali ambavyo huwa na kazi katika mwili wake.

“Kazi moja wapo ya chakula tumeshasema ni kuukinga mwili dhidi ya magonjwa hivyo ukiwa na lishe nzuri utaweza kupambana na maradhi mbalimbali.

“Kama tunavyokwenda vitani mtu mwenye jeshi zuri na askari hodari ndio wanaoshinda vita, ndivyo katika mwili ukiwa na kinga nzuri utaweza kupambana na magonjwa yote nyemelezi, hivyo ni muhimu mtu kula chakula kizuri chenye virutubisho,” anasema.

 

 






Comments 9


  • Awesome Image
    Andrew Mpemba

    Good work kaka mkubwa soon tunafika tunapopataka

  • Awesome Image
    Queen Labab

    Frank anaweza na pia anavipaji mbalimbali nikumsupport Tu ili akamalishe Malengo yake na afike pale anapopatamani, Mungu msaidie🙏🙏

  • Awesome Image
    Maswi mwitha

    Jamaaa nifundi kinomaa namkubari sana kama vip aitwe simba tu akacheze hata namba ya mugalu

  • Awesome Image
    Maswi mwitha

    Jamaaa nifundi kinomaa namkubari sana kama vip aitwe simba tu akacheze hata namba ya mugalu

  • Awesome Image
    Queen Laban

    Mungu ni mwema utashinda na utafikia Malengo yako

  • Awesome Image
    Jek👑

    All the best champ💪ishi ndoto zako

  • Awesome Image
    Jek👑

    All the best champ💪ishi ndoto zako

  • Awesome Image
    Miss project

    Keep it up bro

  • Awesome Image
    Miss project

    Keep it up bro

Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags