Zifahamu changamoto za kazi za kujiajiri mwenyewe

Zifahamu changamoto za kazi za kujiajiri mwenyewe

Naam!! Tumekutana tena hapa hapa waungwana wenzetu kuyajadili yale yote usio yafahamu kuhusu kazi, nikutoe tu hofu sisi Mwananchi Scoop lazima tukwambie kitu cha msingi katika kazi.

Leo katika segment yetu ya kazi tutazungumzia changamoto zinazo wakumba wafanyakazi walio jiajiri wenyewe.

Wengi wetu tumekuwa tukisema faida tu za kujiajiri wenyewe nakuona kwamba ukijiajiri ndio umemaliza kwamba hakunakitu kitakuumiza kwasababu haupangiwi na mtu unajiamulia mwenyewe.

Sasa ngoja nikwambie kitu mwanetu kwa taaarifa yako kuna wakati mwengine ni bora ya huyo bosi wako hapo ofisini anae kusimamia kila wakati kuliko kujisimamia mwenyewe.

Kwanza kunahitaji weledi mkubwa sio rahisi kama unavyo fikiria na ndio maana kabla haujaanza kujiajiri unatakiwa uwemtafiti na mjuzi wakuisimamia ajira yako.

Lasivyo ofisi yako utaifanya kama shamba la bibi ukichukulia mambo kwa urahisi you have to be serious on this dear bila hivyo utapoteza na kukumbuka ajira yako katika ofisi Fulani kwasababu wapo watu wengi wanaanzisha kitu na kina washinda.

Tena sasahivi imekuja tabia ya mbona Fulani amejiajiri na mambo yake yanaenda waswahili wanasema ‘sio kila kitu kinachong’ara ni almasi’ Maana yake ni kuwa kuna ugumu na changamoto kwenye kujiajiri na Mwananchi Scoop iko tayari kukujuza kama ifuatavyo twende kazi sasa. 

  • KUWA NA UHURU MWINGI USIO KUWA NA MSINGI

Hakuna mtu wa kukuamsha, kukumbusha kuhusu kazi za kufanya au mda wa kufanya, unajisimamia kwenye kila kitu ukifanyacho hapa tuwekane sawa kama nilivyo kwambia awali kheri ya kusimamiwa kuliko kujisimamia.

Hivi ulishawahi kujiuliza ukiwa unafanya kazi za watu ofisini unaweza ukawa umechoka au unaumwa lakini bado ukaambiwa ufanye kazi pengine baadae ikaja kuonekana impact nzuri ya hiyo kazi hii inamaanisha kwenye kutafuta kunahitaji ujasiri na uvumilivu ufikie lengo.

Na ndicho kinachotakiwa kufanya hata kwenye kujiajiri kwako lakini sasa iliuone kama ulikuwa unafanya kazi kwa uoga wakufukuzwa kazi basi mtu kwenye ajira yake anaamua kubweteka kwa kuwa hamna mtu wa kumgombeza kumbe muda huo unajipotezea malengo yako.

  • KUWA NA UHAKIKA USIOKAMILI.

Kwa mfano kwenye biashara yaani mpaka utakapofika kiwango cha kuwa na wateja wengi, wanaorudi mara kwa mara, utakuwa na hofu ya kutokuwa na biashara iliyosimama.

Yaani kipindi watu wanajua kuwa unauza bidhaa Fulani wakati huo biashara itakuwa inaelekea kufa kwasababu ulichukua muda mrefu kuwatafuta wateja mpaka mtaji umekula.

Na hata utakapokuwa na wateja wengi, kutakuwa na kipindi ambacho biashara itakosa wateja kwa maana kunakipindi wateja wanakuwa hakuna.

Kutokana na hali ya uchumi sasa hapa ndio ule muda wa kuumiza kichwa ufanye nini ili ulinde ajira yako ulio jiajiri.

  • KUWA NA WATEJA WANAOJIONA.

Kama ulikuwa unamkwepa bosi wako kwa kujiona, maneno yakejeli, ukali na dharau unakuja kukutana na kichefu chefu cha wateja wanaojiona.

Hapo lazima uwe mpole ili upate pesa ya mteja yaani tu nikwambie mteja wako ndio bosi wako sema tofauti tu hujui nani bosi wako wasiku hiyo ukilinganisha na ofisini unajua kila siku bosi wako Fulani.

Muogope mtu ambae huijui tabia yake kuliko ule ambae ni bosi wako kipindi unaajiriwa na ulisha mzoea na tabia zake unazijua.

Pia tegemea kukutana na watu wanaohitaji huduma au bidhaa yako ambao watajiweka kama wanakusaidia kwa kuwa wateja wako, kitu hiki kitatokea sana pale unapowasiliana na hawa watu ili kupata mawazo yao.

  • INACHUKUA MDA SANA KUWA KAMA WAFANYA KAZI WENGINE

Usikae ukategemea kuwa pale utakapofungua ofisi yako, wateja watapigana kama kwenye daladala la Buza na Makumbusho.

Mara nyingi, itakuchukua muda kusimama na kufika kiwango unachokitegemea unatakiwa kuwa mpole mwanetu, chapa kazi, kuwa jasiri na mvumilivu baada ya mda vitu vitakaa vizuri.

Lakini wengi wao hapa uvumulivu unawashinda kwakuwa walizoea kuagizwa na mabosi kazini na kutekeleza basi mwisho wasiku bosi apate hasara au apate faida yeye haimuhusu ilimradi maokoto yake yanaingia kila mwisho wa mwezi anashida gani,

Sasa huwezi kufanya hivyo kwenye ofisi yako hapo ndipo utakapojua bosi wako wa zamani alikuwa anaingiza hasara kiasi gani na alikuwa anauvumilivu hata yeye asipo ingiza pesa atakopa kwenye mabank makubwa na kujirundikia madeni ili wewe upatemshara kwa wakati.

Kipindi hicho wewe ukiambiwa ofisi haijaingiza kitu unakuja juu haulewi kwasababu sio kampuni yako.

Ninachotaka kukwambia mwanetu kila kazi ina ugumu wake iwe ya kuajiriwa au kujiajiri mwenyewe usikae ukabweteka kusiliza watu wakikwambia bora kujiajiri unakuwa na uwamuzi wako hapo kumbuka katika kujiajiri una malengo pia unayatimizaje kama sio kupitia magumu.

Unachotakiwa kama unapojiajiri weka effort vile vile kama umeajiriwa na mtu binafsi chukua hiyo mtu wangu itakusaidia.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post