Zai wa kijiwe Nongwa alamba ubalozi

Zai wa kijiwe Nongwa alamba ubalozi

Alooooh kipo cha kujifunza kutoka kwa mwanadada maarufu anayefanya vichekesho hususani mambo yanayotokea uswahilini,hatimaye amepata ubalozi wa lotion ya kupaka inayoondoa nywele au vinyweleo katika mwili.


Ubalozi huo ameupata kupitia msomi wa Masters, Zawadi Zakaria Masanja ambaye ni Mkazi wa Dar es salaam ameamua kuja na mbadala wa kutumia wembe wakati wa kufanya usafi wa mwili badala yake utatumia lotion kupaka sehemu unayotaka kutoa nywele au vinyweleo kisha kunawa na maji.

Aidha Zawadi alipata ujuzi huo kupitia mtandao baada ya kutafuta kazi kwenye Ofisi mbalimbali kwa muda mrefu bila kufanikiwa.

Hata hivyo Zawadi amenukuliwa akisema  kuwa “Imekuwa ni ndoto yangu ya muda tangu nikiwa masomoni China kufikiria ni kipi nitakileta kwa Jamii yangu kinipe kipato bila ya kuajiriwa, baada ya kutuma maombi ya ajira bila mafanikio nikaanza kujifunza mbinu za usafi wa mwili mtandaoni, niligundua madhira wanayopitia Wnaawake na Wanaume wakati wa kujisafisha”.

“Ikumbukwe kuwa bidhaa hii inatumiwa na watu wote bila kujali jinsia zao  furaha yangu ni kuona baada ya kukosa kazi za maofisini leo nimeleta ajira sio tu kwangu na hata kwa wengine”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags