Yesu wa Tongaren yupo huru sasa

Yesu wa Tongaren yupo huru sasa

Eliud Wekesa maarufu kama Yesu wa Tongaren ameachiwa huru na mahakama baada ya upande wa mashtaka kusema hawana ushahidi wa kuendelea kumshikiria dhidi yake.

Tongareni ambae ni kiongozi wa Kanisa la New Jerusalem Church, amekaa siku tano kizuizini mwa polisi huku maafisa wa upelelezi wakichunguza madai ya makosa dhidi yake yakiwemo shughuli za kidini.

Alishtakiwa kwa kuendesha dhehebu la kidini huko Tongaren akidai kuwa yeye ni Yesu Kristo kufundisha mafundisho ya itikadi kali kwa wafuasi wake ambao baadhi yao ni watoto wadogo na pia utakatishaji fedha.

Aidha baada ya uchunguzi wa kina upande wa mashtaka ulihitimisha kuwa Yesu wa Tongaren Eliud Wekesa hana kesi ya kujibu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags