Yemi Alade amjia juu shabiki yake

Yemi Alade amjia juu shabiki yake

Mwanamuziki Yemi Alade amjia juu mtumiaji wa Twitter aliyemuumbua kuhusu kuchanika kwa mavazi yake kwenye moja ya post aliyoiweka katika mtandao huo.

Picha hizo ziliambatana na ujumbe wa kujigamba kwa kusema kuwa Mimi ni mrembo, mwenye kipaji cha hali ya juu, mkarimu na wa kipekee, unaweza kunidhania ni malaika.

Ndipo mtumiaji huyo wa Twitter anaetumia jina la Darasimi akachukua picha moja na ku-zoom sehemu hiyo na kui-post akiuliza ni mimi pekee ndio nimeona hii?.


Basi bwana waswahili wanasema mchuzi wa mbwa uunywe ukiwa wa moto Mama Afrika akamjibu kwa kusema kuwa…
“Picha hii iliwekwa dakika 3 zilizopita na huo ulikuwa muda wa kutosha kwako kuzoom na kutweet ujinga wako, fikiria kama ungezingatia undani wa maisha yako kwa namna hii, ungekuwa mahali pazuri zaidi ya sasa” ameandika Yemi Alade






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags