Yapi maoni yako juu ya upakaji make up kwa wanawake

Yapi maoni yako juu ya upakaji make up kwa wanawake

Wanawake na mabinti wengi wamekuwa wakitumia urembo wa make up kupaka kwenye nyuso zao kwa lengo la kupata muonekano tofauti, hasa wakienda kwenye masherehe au kwenye kazi zao.

Kutokana na urembo huo baadhi ya wanaume wamekuwa wakichukizwa na ubadilishwaji wa muonekano wa sura unaosababishwa na make up, huku kwa upande wa wanawake wao wanaamini kuwa upakaji wa urembo huo husaidia kuwaongezea mvuto.

Kutokana na upakaji make up kwa wanawake Mwananchi Scoop imefanya mahijiano na baadhi ya wanaume kutaka kufahamu nini maoni yao juu ya urembo huu.


Goodluck John kutoka Zanzibar yeye ameweka wazi kwa kusema, “Kwanza kwa upande wangu sipendi mwanamke anayepaka make up, nachukia kutoka moyoni mwangu na jambo linalonifanya nichukie ni kuwa sipendi mtu asiyejiamini na kujikubali nikisema hivi naeleweka, wanawake wengi wanapaka make up wakijua wanatuvutia lakini wangejua mioyoni mwetu wasingeendelea kutipaka hizo make up zao”. Anasema

Aidha kwa upande wake Bakari Said anasema,
“Kwa upande wangu siyo kama nachukia sichukii, ila sipendi mwanamke anayejiweka mavumbi yale, mbona wapo wanaopaka wanja, ‘maskala na wanapendeza tu bila shida kiufupi niwashauri wanawake kupunguza kupaka make up , kwa sababu wanaume wengi hatupendezwi nayo tunashindwa tu kuwaambia ukweli, hukatazwi kupaka ila paka kidogo na siyo kila siku”

Yapi maoni yako juu ya upakaji make up kwa wanawake?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post