Yammi awajia juu wanao msema kuhusu mavazi yake

Yammi awajia juu wanao msema kuhusu mavazi yake

Nyieee!! Amkeni huku kumekucha bhana hili suala la uvaaji wa mwanamuziki Yasiruni Yasini Shabani maarufu Yammi umevuka mipaka mpka mashabiki mitandaoni wanamsema vibaya msanii huyo.

Ikumbukwe tu hapo mwanzo mwanadada huyo kabla hajatoa hit song alikuwa na maadili flani hivi ya kiislam ushungi mwingi lakini now amebadilika amekuwa na mavazi flani hivi ya kina Kim Kardashian.

Team ya Mwananchi Scoop hatukulikalia kimya swala hili tuka mvutia waya mwanadada Yammi akaingia laini bhana na kufunguka kuhusu uvaaji wake.

 “Ukiwa msanii lazima uwendane na system iliopo siwezi nikawa na imba huku nimevaa vishungi watu watakuwa hawanielewi na kwangu mimi sioni tatizo lolote na vaa kama wanavyo vaa wasanii weningine”alisema Yammi.

Pia alizungumza ishu ya kuchaguliwa nguo ambazo atavaa katika nyimbo yake au shows mbalimbali amesema kuwa “Hapa inategemea na tukio naweza kuchagua mwenyewe, style au Nandy vyovyote inategemea na tukio”alisema Yammi

Hahahaha sambamba na hayo bhana jana katika show ya Serengeti lite alipata fursa ya kutumbuiza sasa kumezuka minong’ono ya watu kuwa vazi alilo livaa stajini lina fananishwa na zulia (kapert) huku na huku kutaka kujua designer wa hilo vazi tukaona isiwe tabu wacha tumuulize mwenyewe dada Yammi

“Siwezi nikamuweka wazi designer wangu nitamharibia itakuwa sio uungwana kwasababu yeye mwenyewe hajaniruhusu nimuongelee mimi mwenyewe niliona liko sawa tuu na sijali watu wanazungumza nini”alisema Yammi

Hahahhahah! Make hapa kwanza ncheke, hivi mmeliona lile kapeti kwanza au niwaache kidogo (jokes), embu tuambie mtazamo wako mwenetu sana kweli lile ni zuria au watu wanazusha, dondosha komenti yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags