Yajue mambo matano muhimu kuhusu shinikizo la damu

Yajue mambo matano muhimu kuhusu shinikizo la damu

Na Elizabeth Malaba

Shinikizo la juu la damu ni moja ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza lakini mtu anaweza  kupata kwa kurithi( genetic hereditary) yawezekana  katika familia kuna historia ya ugonjwa huu wa shinikizo la damu, ambapo ugoniwa huu unashika kasi saana na kumekuwa na ongezeko la wagonjwa wa shinikizo la damu, hii yote ni kutokana na mfumo mzima wa maisha yetu ya kisasa.

Zamani tulizoea kuwaona wazee au watu wenye umri mkubwa kusumbuliwa na ugonjwa huu wa shinikizo la damu lakini kwa sasa mambo yamebadilika hata watoto wadogo wamekuwa wakisumbuliwa pia, hii ni kutokana pia na wazazi kupendelea kuwalisha watoto vyakula vyenye makemikali mengi (hasa vya supermarket).karibu tujifunze mambo muhimu kuhusu ugonjwa wa shinikizo la damu:

Shinikizo la juu la damu ni ugonjwa unaotokana na msukumo wa damu unapokuwa juu ya kiwango cha kawaida katika mishipa ya damu mwilini.

Shinikizo la juu la damu hujukikana kwa kitaalamu kama Hypertension. Kwa kawaida shinikizo la damu linatakiwa kuwa 110/70mmg-120/80mmg.

Mara nyingi wagonjwa wa shinikizo la juu la damu hawana dalili zinazoashiria kuwa na tatizo  hilo, kwa kawaida wagonjwa wengi hugundulika kuwa na tatizo la shinikizo la juu la damu katika uchunguzi wa kawaida tu wa magonjwa mengine wanapokuwa hospitalini.

Lakini pia kumbuka kwamba shinikizo la damu linaweza kuwa juu kutokana na baadhi ya matukio kama vile hofu, mazoezi nk.

Takwimu za Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) zinasema tayari watu bilioni moja duniani kote, wanaathiriwa na shinikizo la juu la damu huku likisababisha mshtuko wa moyo (Heart attacks), kupooza na kiharusi (Stroke). Shinikizo la juu la damu huwapata zaidi wanaume kuliko wanawake.

Sababu na vihatarishi vya shinikizo la juu la damu:

Yafuatayo ni baadhi ya sababu  zinazoweza kupelekea mtu  hatarini  kupata shinikizo la juu la damu ambayo ni pamoja na;

  • Umri mkubwa zaidi ya miaka 65.
  • Kuwa na unene uliopitiliza (obesity).
  • Uvutaji wa sigara na ulevi kupindukia.
  • Magonjwa ya figo (renal diseases).
  • Kuwa na ndugu wa damu wenye matatizo ya presha (family history of hypertension).
  • Ugonjwa wa kisukari.
  • Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).

Dalili za shinikizo la juu la damu.

  • Zifuatazo ni dalili za shinikizo la juu la damu ambazo ni pamoja na;
  • Kizunguzungu (dizziness).
  • Mapigo ya moyo kwenda mbio (palpitation).
  • Kuchoka mara kwa mara (easy fatigability).
  • Maumivu ya kifua (chest pain).
  • Maumivu ya kichwa (headache).
  • Uonaji hafifu (blurred vision).

Kumbuka: Uonapo dalili hizi unapaswa kuwahi hospitali kupata vipimo.

Matibabu ya shinikizo la juu la damu:

Tiba ya shinikizo la juu la damu hutegemea na chanzo cha shinikizo kwa mtu uyo ni kipi. Chanzo kikijulikana na kikafanyiwa marekebisho au maboresho huwa ni bora zaidi.

Kwa upande wa hospitali kuna dawa kadhaa ambazo hutumika kushusha shinikizo laa juu la damu ambazo hujulikana kwa kitaalamu kama Anti-hypertensive drugs na huchaguliwa kwa mhusika atumie ipi hasa kwa kuzingatia vigezo kama umri, afya yake, hali ya moyo, magonjwa mengine ambatano mwilini kama vile magonjwa ya ini, figo, kisukari nk.

Dawa hizo ni kama vile;

  • Thiazides mfano Benzothiadiazine, chlorothiazide.
  • Diuretics mfano Furosemide (lasix).
  • Beta blockers mfano Propranolol, atenolol, metoprolol.
  • Calcium channel blockers mfano Amlodipine, nifedipine.
  • Angiotensin Converting Enzymes (ACEIs) mfano Captopril, Enalapril.

Kumbuka: Dawa hizi uhitaji umakini mkubwa na mgonjwa anatakiwa kuzitumia sehemu kubwa ya maisha yake. 

Madhara ya shinikizo la damu:

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea kwa mgonjwa mwenye shinikizo la juu la damu ikiwa atashindwa kupata matibabu mapema;

  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure).
  • Moyo kutanuka.
  • Shambulio la moyo.
  • Kuharibu figo na figo kushindwa kufanya kazi.
  • Kusababisha upofu.
  • Kipanda uso (migraine headache).

Na vifuatavyo ni baadhi ya vyakula anavyoshauriwa kula mgonjwa mwenye shinikizo la juu la damu ambavyo ni pamoja na;

  • Samaki

Samaki ni chanzo kikubwa cha protini mwilini, mfano samaki wa aina ya salmon ni chanzo kizuri cha kemikali iitwayo omega-3 ambayo husaidia kushusha shinikizo la juu la damu kwa kupunguza kiwango cha cholesterol kwenye mishipa ya damu.

  • Mboga Za Majani.

Mboga za majani zenye kiwango kikubwa cha madini ya potasium kama vile spinachi, bamia, mchicha, chainizi husaidia kupunguza kiwango kikubwa cha chumvi (sodium) kwenye damu ambayo ni mojawapo ya kisababishi cha kupanda kwa shinikizo la damu kwa hawa wagonjwa.

  • Mbegu Za Maboga.

Mbegu za maboga ni chanzo kikubwa cha madini ya potasium na magnesium ambayo husaidia kupunguza kiwango kikubwa cha chumvi, sodium kwenye damu na hivyo kushusha shinikizo la juu la damu kwa hawa wagonjwa.

  • Vitunguu Swaumu.

Vitunguu swaumu ni chanzo kikubwa cha kemikali iitwayo nitric acid ambayo inafanya kazi ya kutanua mishipa ya damu, hii huongeza nafasi kubwa kwa ajili ya kupitisha damu vizuri kwenda sehemu mbalimbali za mwili bila kuongeza shinikizo la damu.

Ndizi Mbivu.

Ndizi mbivu ni muhimu sana kwa mgonjwa mwenye shinikizo la juu la damu kwani zina kiwango kikubwa cha madini ya potasium ambayo husaidia kupunguza kiwango kikubwa cha chumvi, sodium kwenye damu ambayo husabisha kupanda kwa shinikizo la damu.

Berries ni aina ya matunda ambayo yana kemikali iitwayo flavonoids ambayo imethibitika kusaidia kushusha shinikizo la juu la damu kwa hawa wagonjwa.

Tangawizi hufanya kazi ya kulainisha damu kwa kupunguza uzito wake na kupunguza shinikizo la juu la damu kwa kiasi kikubwa kwa hawa wagonjwa. Unashauriwa kutumia unga wa tangawizi kwenye chai yako kila siku badala ya kutumia majani ya chai ambayo kiafya hayana faida yoyote.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post