Xavi bado yupo sana Barcelona

Xavi bado yupo sana Barcelona

Baada ya kutangaza kuondoka mwishoni mwa msimu katika klabu ya #Barcelona, kocha #XaviHernandez amebadili msimamo wake kwa kuthibitisha kuwa atabaki klabuni hapo hadi mwisho wa mkataba wake.

Kwa mujibu wa Sky Sport News imeeleza kuwa kocha huyo amedai kuwa sasa anaona kabisa hajatimiza malengo yake na itakuwa siyo sawa kuondoka katika timu hiyo kabla ya mkataba wake kutamatika

Hivyo kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 amesema kuwa amebadili msimamo wake wa mwanzo na hata angeondoka asingechukua kiasi chochote cha fedha kama fidia ya kuvunja mkataba wake.

Awali viongozi wa klabu hiyo hawakuonesha nia ya kuendelea na Xavi hivyo walikubaliana kuacha kuifundisha klabu hiyo na kukatisha mkataba wake ambao unamalizika mwaka 2025.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags