Wolper, Batuli, Wema, Wamlilia aliyekuwa mpiga picha wa Millard Ayo

Wolper, Batuli, Wema, Wamlilia aliyekuwa mpiga picha wa Millard Ayo

Mpiga picha na mwandishi wa habari wa #Millardayo Noel Mwingila maarufu kama Zuchy amefariki dunia leo Alfajiri baada ya kupata ajali ya pikipiki maeneo ya Mbezi Makonde Jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wasanii ambao aliwahi kufanya nao kazi akiwemo Wema Sepetu, Batuli Actress, Jackline Worlper wameonesha kusikitishwa na kifo cha kijana huyo.

Kwa upande wa Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika, “Daaaaaah Speechless rest in peace Zuchy, hii hali inatisha”. Akimaanisha sina cha kuongea pumzika kwa amani Zuchy

Hata hivyo Batuli Actress ameandika kuwa Mungu ndiye mwenye kumiliki na ndiye aliyeamua kumchukua kijana huyo.

“Mwenye nguvu, mwenye maamuzi, mwenye kumiliki na muweza wa yote kaamua tena kwa Zuchi naandika na kufuta zaidi ya nusu saa, Zuchy kwa hiyo juzi ulikuwa unaniaga mdogo angu, Mungu naomba tusamehe” ameandika Batuli.

Naye Jackline Wolper ametoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki akitaka Mungu awasamehe askari waliomuacha katika mvua baada ya ajali kutokea.

“ Rafiki yangu pole ndugu jamaa na marafiki wote na Mungu awasamehe polisi waliokuacha kwenye mvua leo nenda rafiki yangu Mungu akupunguzie adhabu mpambanaji wangu” ameandika Wolper.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags