Wolper, Aahidi kuzungumza siku ya harusi  yake

Wolper, Aahidi kuzungumza siku ya harusi yake

Aloooh! Ndugu yangu vipi unapicha ya kumbukumbu ya kututolea stori siku yako ya kuoa/kuolewa au upo upo tuu hahaha! sasa bwana msanii wa bongo movie Tanzania Wolper Amesema ataweka wazi na kutoa maelezo yanayo eleweka kuhusiana na picha alio iposti katika siku yake ya muhimu ya harusi.

Wolper ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kueleza kuwa “nina story ndefu juu ya hii picha ila nitaongea kwenye harusi yangu in shaa allah!, nitaeleza kila kitu kwa wageni waalikwa pale kwenye hitimisho letu” ameseme Wolper

Aidha muigizaji huyo aliendelea kwa kufunguka kuwa “huu ulikuwa ni mwaka 2016 ndani ya China na hii picha imepigwa na Rich Mitindo ambaye atukujua kama mungu katupangia nini, eti sasa hivi namuita Baba P yaani mume wangu mtarajiwa, sifa na utukufu ni kwako bwana mwokozi wetu” amesema Wolper

Eeeeeh! Haya wewe na huyo mwenzio mnachakutuambia siku yenu ya harusi au ndo tutakula na kucheza tu hahahah! sio shida zenu, dondosha koment yako hapo chini mwanangu sana






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags