Wizkid: Sasa nampenda mungu, Sina chuki na mtu

Wizkid: Sasa nampenda mungu, Sina chuki na mtu

Baada ya bifu la mwanamuziki Wizkid na Davido kulindima kwa wiki kadha, hatimaye Wizkid amedai kuwa kwa sasa anampenda Mungu na hana chuki na mtu yeyote.

Wizkid ameyasema hayo kupitia mtandao wa X (zamani Twitter) alipokuwa akijibu madai ya baadhi ya watumiaji wa mitandao huo kwamba tweets zake za hivi karibuni zilikuwa zikimlenga msanii mwenzake Davido

Hata hivyo msanii huyo ameeleza kuwa hana chuki na mtu yeyote, huku akisisitiza kuwa anamtakia kheri kila mtu na kuhusu mambo anayopost kwenye mtandao huo ni kwa ajili ya kujifurahisha huku akiwataka watu kutoyachanganya na maisha yake.

Wiki chache zilizopita Wizkdi kupitia mtandao huo amekuwa akirusha madongo ambayo yalizua utata huku baadhi ya mashabiki wakidai kuwa maneno hayo yalikuwa yakimlenga Davido.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags