Wimbo wa nay amkeni wapigwa stop

Wimbo wa nay amkeni wapigwa stop

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imetoa katazo kwa wimbo wa msanii wa #Hiphop  Nay wa Mitego, 'Amkeni' kupigwa kwenye Vyombo vya Habari na mitandao ya kijami.

Kupitia ukurasa wa twitter wa Nay ame-share picha ya barua inayotoa maelekezo ya wimbo wake kutopigwa kwenye Vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii huku barua hiyo ikionesha kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bw. John Daffa.

Kwenye barua hiyo inaeleza kuwa kwa mujibu wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), wimbo huo wa Ney unataka wananchi wasiwe na imani na serikali, na kuchochea matokeo hasi juu ya utekelezaji wa mipango ya serikali kwa ujumla.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags