Wimbo wa Kendrick Lamar wazua kizaazaa

Wimbo wa Kendrick Lamar wazua kizaazaa

Shule ya ‘Vernon Center Middle School’ iliyopo jijini Manchester imekubali kulipa fidia ya dola 100,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 263 milioni baada ya mwanafunzi wa shule hiyo kudai kufadhaika kihisia kutokana na wimbo wa Kendrick Lamar wa ‘Alright’ uliochezwa darasani.

Kesi hiyo, iliyowasilishwa mwaka wa 2022, ilidai kuwa Februari 12, 2020 mwalimu wa somo la kijamii aitwaye Owens alionesha video ya wimbo wa Lamar bila idhini ya wanafunzi.

Video ya wimbo huo mwishoni ilionesha ‘rapa’ huyo akipigwa risasi na polisi jambo ambalo lilipelekea mmoja wa wanafunzi kupata mfadhaiko.

Familia ya mwanafunzi huyo ambaye hakuwekwa wazi jina lake ilieleza kuwa mwalimu Owens kuonesha video ya wimbo huo ilikuwa kama anafikisha ujumbe kwa mwanafunzi huyo ambaye baba yake alikuwa ni polisi mstaafu.

Kesi hiyo inadai kuwa video ilionesha maafisa wa polisi kama wauaji na ilikuwa na matukio mengine ya vurugu na taarifa za kutatanisha kuhusu maafisa wa polisi.

Wimbo huo wa Lamar uliachiwa rasmi Machi 15, 2015 na uliteuliwa kuwania tuzo nne za Grammy na kushinda Best Rap Performance na Best Rap Song.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post