Kampuni ya mtandao ya Whatsapp yapigwa faini ya Tsh. bilioni 13.9 kwa kukiuka sheria ya ulinzi wa taarifa binafsi za watumiaji wao.
Tume ya Kulinda Data ya Ireland (DPC) imetoa adhabu hiyo baada ya kubaini ukiukaji wa majukumu yake na kutoweka wazi matumizi ya taarifa binafsi inazokusanya kutoka kwa watumiaji wake.
DPC ambayo inafanya kazi kama mdhibiti mkuu wa faragha wa umoja wa Ulaya (EU), imeitaka WhatsApp kujitathmini jinsi inavyotumia na inazilindaje taarifa binafsi za wateja.
Ni wiki 2 tangu Umoja wa Ulaya uitoze faini ya Tsh. Bilioni 961 kwa Mitandao ya Facebook na Instagram kwa kulazimisha watumiaji kuona matangazo yanayoendana na utafutaji mtandaoni. META inakabiliwa na kesi nyingine 10 za ukiukaji wa sheria za data binafsi.
Leave a Reply