WhatsApp kuwezesha utumaji ujumbe bila bando

WhatsApp kuwezesha utumaji ujumbe bila bando

Huduma ya kutuma ujumbe papo hapo ya  WhatsApp itawaruhusu watumiaji kuunganishwa kupitia seva mbadala ili waweze kusalia mtandaoni ikiwa mtandao utazuiwa au kukatizwa na kuzimwa.

Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia, inayomilikiwa na Meta, ilisema inatumai kukatika kwa huduma za mtandao kama vile huko Iran hakutatokea tena.

Ambapo waliwanyima watu haki za binadamu na "wakakata watu kupokea msaada wa haraka".

WhatsApp jamii yake ya kimataifa kujitolea kusaidia watu kuwasiliana kwa uhuru na ilisema itatoa mwongozo wa jinsi ya kuanza kufanya hivyo.

"Kuunganisha kupitia seva mbadala kunadumisha kiwango sawa cha faragha na usalama ambacho WhatsApp hutoa, ilisema katika blogi yao.

"Ujumbe wako wa kibinafsi bado utalindwa kwa usimbaji fiche kutoka mwanzo hadi mwisho - kuhakikisha kuwa unasalia kati yako na mtu unayewasiliana naye na hauonekani na mtu yeyote kati yao, sio seva mbadala, WhatsApp au Meta."

Juras Juršėnas, kutoka wakala na kampuni ya ukusanyaji wa data mtandaoni ya Oxylabs, aliiambia bbc "Kwa watu walio na vikwazo vya serikali katika upatikanaji wa mtandao, kama ilivyokuwa kwa Iran, matumizi ya seva mbadala yanaweza kuwaruhusu watu kudumisha uhusiano na WhatsApp na maeneo mengine ya mtandaoni. mtandao wa bure, ambao haujadhibitiwa.

"Itawaruhusu watu kote ulimwenguni kusalia wameunganishwa hata ikiwa ufikiaji wao wa mtandao umezuiwa’

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags