Wembe uliosahaulika tumboni mwa mwanamama Felistah waondolewa

Wembe uliosahaulika tumboni mwa mwanamama Felistah waondolewa

Madaktari nchini Kenya wameondoa wembe unaodaiwa kusahaulika ndani ya tumbo la mwanamke kwa takriban miaka 11, gazeti la Daily Nation nchini humo limeeleza.

Tatizo hilo lilianza wiki kadhaa baada ya kufanyiwa upasuaji wa kujifungua (caesarian ama C-Section) mtoto wake wa kwanza katika hospitali ya Kitale, magharibi mwa Kenya.

Kwa miaka 11, Bi Felistah Nafula, mwenye umri wa miaka 36, amekuwa akiishi na maumivu ya tumbo ambayo aliamini ni vidonda vya tumbo na amekuwa akipata matibabu ya ugonjwa huo.

Kadri miaka ilivyokwenda huku alihisi maumivu makali, madaktari walianza kushuku kwamba tatizo lilikuwa kubwa kuliko ugonjwa wa vidonda vya tumbo (ulcers).

Aidha vipimo kadhaa vya scan vilionyesha kuwa vilisababishwa na kitu cha chuma tumboni mwake na hivyo alikwenda katika hospitali ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Maragua Level Four katika kaunti ya Murang'a.

Baada ya kufanyiwa upasuaji wa saa 2, Alhamisi, madaktari walibaini wembe wa upasuaji ndani ya tumbo lake.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags