Wazazi walia na walimu kuwageuza wanafunzi kuwa wapenzi wao, Tabora

Wazazi walia na walimu kuwageuza wanafunzi kuwa wapenzi wao, Tabora

baaadhi ya walimu Wilayani Kaliua mkoani Tabora wamelalamikiwa na wazazi pamoja na walezi kwa kuwalaghai wanafunzi hao kwa kufanya nao mapenzi na kisha kupata ujauzito.

malalamiko hayo yametolewa mbele ya katibu wa Halmashauri kuu ya chama cha CCM itikadi na uenezi, Shaka Hamidu katika ziara yake mkoani humo.

akizungumza mmoja wa wazazi hao alifunguka na kueleza kuwa kuna baadhi ya walimu wa shule ya Sekondari Mwongozo hufanya mapenz na wanafunzi hadi kupata ujauzito pasipo kuchukuliwa hatua yoyote " kuna mwalimu kakamatwa  akiwa anafanya mapenzi na mwanafunzi lakini katoroka na hajakamatwa hadi leo na sio huyo peke yake kuna walimu wengi wenye tabia za namna hiyo kiongozi tunaomba utusaidie" amesema mzazi huyo

aidha mkuu wa Wilaya hiyo Paul Matiko alijibu malalamiko hayo na kusema kuwa kweli kuna baadhi ya walimu wenye tabia hizo na tayari hatua stahiki kwa baadhi ya walimu hao zimechukuliwa hivyo swala lenu linafanyiwa kazi.

hata hivyo Shaka amemwagiza mkuu wa Wilaya hiyo kuwasaka walimu wanaolalamikiwa kujihusisha na vitendo hivyo na kuhakikisha wanapekelekwa sehemu husika na kupata adhabi inayo wastahiri






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags