Watu sita wafariki katika maandamano kuhusu uvaaji wa hijabu

Watu sita wafariki katika maandamano kuhusu uvaaji wa hijabu

Idadi ya waliokufa katika maandamano yanayoendelea nchini Iran imeongezeka na kufika watu sita. Maandamano hayo ambayo yamekuwa yakiendelea mfululizo tangu Ijumaa yamefuatia kifo cha msichana mwenye umri wa miaka 22, Mahsa Amini, kilichotokea mikononi mwa polisi wa maadili, akituhumiwa kuvaa hijabu katika mtindo usiostahili.

Baadhi ya wanawake katika maandamano hayo wamevua hijabu zao kwa ukaidi na kuzichoma moto mbele ya umati unaoshangilia. Shirika la habari la serikali ya Iran limesema kuwa maandamano hayo yameenea katika miji 15 na polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji.

Aidha Shirika la haki za binadamu la Article 19 limeituhumu polisi wa Iran kutumia nguvu za ziada dhidi ya waandamanaji, ikiwemo risasi za moto.

Katika hotuba yake mbele ya hadhara kuu ya Umoja wa Iran, rais wa Iran, Ebrahim Raisi amepuuza ukosoaji unaotolewa na nchi za magharibi, akizituhumu kuwa na undumilakuwili.

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post