Watu 76 wauawa katika ajali ya boti nchini Nigeria

Watu 76 wauawa katika ajali ya boti nchini Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amesema kuwa karibu wasafiri wote waliokuwa katika boti iliyopinduka kwenye mto Niger wamefariki. Wafanyakazi wa huduma za uokozi wa dharura wamethibitisha vifo vya watu 76 kati ya 85 wanaoripotiwa kuwa katika boti hiyo ilipopata ajali.

Taarifa ya Ikulu ya Rais Buhari imemnukuu kiongozi huyo akiwaombea dua waliopoteza maisha na kuzitakia afueni familia zilizopoteza wapendwa wao na kuhimiza idara zinazohusika kuzifariji familia hizo.

Mratibu wa huduma za dharura ngazi ya taifa kusini mwa Nigeria, Thickman Tanimu amesema sababu ya ajali hiyo ni kuongezeka sana kwa kina cha maji ya mto Niger katika eneo la Ogbaru ambayo pia imetatiza shughuli za uokozi.

Boti hiyo ilipinduka Ijumaa iliyopita.

Inariporiwa kuwa ajali za majini hutokea mara kwa mara nchini Nigeria kutokana na vyombo kupakia abiria kuliko uwezo wake, kasi kubwa, uchakavu wa vyombo hivyo na kutojali kanuni za usafiri wa majini.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags