Watu 19 wafariki nchini Morocco baada ya kunywa pombe yenye sumu

Watu 19 wafariki nchini Morocco baada ya kunywa pombe yenye sumu

Takriban watu 19 wamefariki na wengine mahututi baada ya kunywa pombe kwenye duka lililopo kando ya barabara katika mji wa kaskazini wa Morocco, Ksar el-Kebir.

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 48 amekamatwa kuhusiana na tukio hilo. Jeshi la Polisi la mji huo wanasema wamekamata lita 50 za pombe kwenye duka hilo.

Licha ya kuuza pombe kwa Waislamu imekatazwa nchini Morocco, lakini mara nyingi huuzwa kwa siri katika migahawa tofauti tofauti ilioko katika mji huo.

Aidha Mwezi Agosti, watu wanane walifariki baada ya kunywa pombe yenye sumu katika jimbo la kaskazini la Oriental na takriban watu 20 walifariki Julai mwaka jana katika tukio sawa na hilo katika mji wa Oujda, mashariki mwa Morocco.

Chanzo BBC


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post