Watu 10 matajiri zaidi kuwahi kuishi duniani

Watu 10 matajiri zaidi kuwahi kuishi duniani

  1. Mansa Musa (1280-1337, Mfalme wa Mali ambaye mali yake haiwezi kuelezewa
  2. Augustus Caesar (63 BC-14 AD, Mfalme wa Roma) $4.6tn (£3.5tn)
  3. Zhao Xu (1048-1085, Mfalme wa Shenzong of Song China) mali yake haikuweza kuhesabika
  4. Akbar I (1542-1605, Mfalme wa Mughal India) mali yake haikuweza kuhesabika
  5. Andrew Carnegie (1835-1919, Mfanyabiashara wa viwanda wa Uskochi na Marekani) $372bn
  6. John D Rockefeller (1839-1937) Mfanyabishara wa Marekani) $341bn
  7. Nikolai Alexandrovich Romanov (1868-1918, Tsar wa Russia) $300bn
  8. Mir Osman Ali Khan (1886-1967, Ufalme wa India) $230bn
  9. William The Conqueror (1028-1087) $229.5bn
  10. Muammar Gaddafi (1942-2011, -Mtawala wa Libya) $200bn

 

Mansa Musa alizaliwa 1280 katika familia ya watawala. Nduguye , Mansa Abu-Bakr, alitawala ufamle huo hadi 1312, wakati alipoamua kwenda safari.

Kulingana na mwanahistoria wa karne ya 14 Shibab al-Umari, Abu-Bakr alipendelea sana kuiona bahari ya Atlantic na kile ilichokuwa nacho.

Aliripotiwa kuanza safari na msafara wa meli 2000 na maelfu ya wanaume na wanawake pamoja na watumwa. Walienda na hawakurudi tena.

Wengine kama vile mwanahistoria wa Marekani Ivan Van Sertima anadai kwamba waliwasili Marekani Kusini. Lakini hakuna ushahidi.

Ukweli ni kwamba Mansa Musa alirithi ufalme ulioachwa nyuma na nduguye. Chini ya uongozi wake ufalme wa Mali uliimarika kwa kiwango kikubwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post