Watatu wakamatwa kifo cha AKA

Watatu wakamatwa kifo cha AKA

Kufuatia mauaji ya rapa kutoka nchini Afrika Kusini, Kierman Forbes maarufu kama AKA, wanaume watatu wameripotiwa kukamatwa kuhusiana na mauaji yaliyotokea February 10, 2023.

kwa mujibu wa tovuti ya habari nchini humo ya IOL, chanzo kilicho karibu na uchunguzi wa mauaji ya rapper huyo kilisema washukiwa hao walikamatwa na polisi mjini Cape Town, siku ya Jumapili, baada ya kuwafuatilia kwa wiki nzima.

Chanzo hicho kilisema washukiwa ambao wako chini ya ulinzi wa polisi watafikishwa Durban ambapo wanatarajiwa kufunguliwa mashtaka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags