Ebwana niaje my beautiful people, its another time bila kupoa katika jarida la Mwananchi Scoop kwenye segment ya burudani na kudondoshea list ya mastaa waliotamba kwenye mziki wa bongo fleva na kutangaza mziki nnje ya mipaka ya Tanzania.
Katika miaka ya 2000 hadi 2007, neno la bongo fleva halikuwa jipya sana katika masikio ya wapenzi wa burudani kwani mzuki huo ulikuwa umeshika hatamu katika vituo tofauti tofauti vya habari vilevile wasanii walitumika kutoa elimu katika jamii kupitia sanaa ya uimbaji,unataka kujua wasanii hao ni wakina nani? Twende pamoja kujua mastaa hao.
RAY C
Ray C kwa jina la kisanii ila jina lake la halisi ni Rehema Chalamila, mwanadada huyu alijizolea umaarufu katika game la muzikii wa bongo fleva chini ya meneja wake mashuhuri marehemu, Ruge Mutahaba.
Katika wakati huo Ray C aliweza kuachia album nne kwa miaka tofauti tofauti ambazo zilimtambulisha kwa mashabiki na baadhi ya nyimbo kama mapenzi yangu, na wewe milele, sogea sogea na touch me ambazo zilizobeba jina katika album hizo kufanya vizuri zaidi.
Msanii huyo aliweza kushiriki na kushinda tuzo za muziki ndani ya nchi na nne ya Tanzania. Baadhi ya tuzo alizowahi kushinda ni ya mwaka 2004 Tanzania Music Award - Msanii Bora wa kike, 2006 Pearl of Africa Music Awards - Msanii bora wa kike (Tanzania) na 2005 Channel O Music Awards - Msanii bora Afrika ya Mashariki.
FEROOZ
Ferooz ndo jina la sanaa na wengi tunamfahamu kwa jina hilo, Mwamba huyu jina lake halisi anafahamika kama Feruzi Mrisho ambaye alifanya harakati zake za mziki akiwa kwenye kundi la Daz Nundaz.
Mwamba huyu alifanikiwa kutoa album yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la starehe. Katika album hiyo, wimbo wa starehe aliomshirikisha Professor Jay ulimletea mafanikio na umaarufu zaidi kutokana na ujumbe wake na mwaka 2005 alijinyakulia tuzo.
CHID BENZ
Rashid Makwiro, maarufu kwa jina la sanaa kama Chid Benz a.k.a chuma, mkali huyu alitamba zaidi kwa wimbo wa ‘Naitwa nani’ mwaka 2006 na nyimbo zingine kama ngoma itambae, mmeisoma.
Pia msanii huyo aliweza kupata tuzo zaidi moja kupitia kipengele cha msanii bora wa Hip hop na wimbo bora. Ifahamike huyu ndo muasisi wa kundi ‘La Familia’ kupitia wimbo wa ngoma Itambae (Dar es salaam stand up) ulioitangaza vyema Ilala na kuendelea kuishi kwenye vichwa vya mashabiki hadi leo.
MANGWAIR
Marehemu Albert Mangwea, ebwana tukimzungumzia muziki wa bongo fleva hutoweza msahau mtaja. Legend huyo ambaye nyota yake katika tasnia ya muziki ilionekana baada ya kuachia wimbo wa ,Ghetto langu, mwaka 2003 chini ya mtayarishaji mahiri wa mziki P Funk Majani.
Msanii huyo aliachia nyimbo nyingine na baadhi ya nyimbo hizo ni Nipe dili, Tuko juu, Sikiliza na Mikasi ambazo zilimzolea umaarufu katika kona zote za Tanzania na kujinyakulia tuzo mbalimbali kama msanii bora wa Hip hop.
MR NICE
Alooh! Huyu ndo yule hit maker wa nyimbo kalii katika miaka ya 2000. Jina kamili la msanii huyu ni Lucas Mkenda ambaye alifanikiwa kutoa baadhi ya album na zilifanya poa sana na miongoni mwa nyimbo zilizomtambulisha katika game la bongo fleva ni kikulacho, fagilia bongo, kidali po na kuku kapanda baiskeli.
Pia msanii huyu aliweza kupata show kwa utunzi wake wa muziki ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
JAY MOE
Juma Mchompanga alifahamika kama Jay Moe (jina la kutafutia riziki) pale alipoachia album yake ya kwanza iliyokwenda kwa jina la ulimwengu mama mwaka 2001.
Kwenye album yake ambayo ilipikwa kwa midundo mikali ya P Funk Majani zilipatikana nyimbo kama mvua na jua, bishoo na kama unataka demu ambazo zilifanya vizuri na kumpa umaarufu na hata kupata show nyingi ndani ya nchi.
PROFESSOR JAY
Joseph Haule ama Professor Jay, jina ambalo wapenzi wengi wa mziki wa bongo fleva tunalijua mara baada ya msanii huyo kusimama kama msanii binafsi mwaka 2001 na kuweza kuachia album yake ya kwanza iitwayo Machozi, Jasho na Damu.
Album yake ilivuma kwa kasi na hata kumfanya achukue tuzo kadhaa kwa kuwa mtunzi bora wa Hip hop kwa wimbo wake wa Ndio mzee, piga makofi na nyimbo zingine zilizomzolea umaarufu kwenye kiwanda cha bongo fleva na kuendelea kubaki kuwa ngoma kali ni zali la mentali, promota anabeep na msinitenge.
LADY JAYDEE
Lady jaydee ama Komando Jidee, jina lake najua sio geni sana kulisikia kwani ni miongoni mwa wasanii wa kike wa mwanzo kurusha karata ya uimbaji katika tasnia ya bongo fleva.
Komando Jidee alianza rasmi safari yake ya mzikii mwaka 2000 na kuachia album yake ya Machozi na kuanza kuachia nyimbo kutoka kwenye album hiyo. Baadhi ya nyimbo alizotoa zilizofanya vizuri ni machozi ya furaha, faraja na distance. Pia alifanikiwa kufanya collabo na wanamuziki wengine na kuendelea kubaki kuwa mkongwe katika tasnia ya bongo fleva kwa wasanii wa kike.
MWANA FA
Mwana Falsafa ila kwenye game la bongo fleva maarufu kama Mwana FA, mkali wa tungo toka miaka ya 2000 alipoamua kuonyesha dunia uwezo wake wa kutunga nyimbo na kurap na kubaki kwenye rekodi ya kuwa msanii wa Hip hop mkongwe.
Msanii huyu aliachia nyimbo kama habari ndo hiyo, alikufa kwa ngoma, unanijua unanisikia na nyimbo nyingine kali ambazo zilimbebea umaarufu kila kona ya Tanzania na kuaminisha jamii muziki wa bongo fleva sio uhuni kupitia utunzi wa nyimbo zake zenye kuelimisha.
DULLY SYKES
Dully Skyes mkali katika game la muzikii kitambo hadi leo bado hachuji na hapoi. Msanii huyu aliingia kwenye kiwanda cha mziki na kuongeza ladha ya namna yake katika utunzi na uimbaji wa nyimbo za zake.
Miongoni mwa nyimbo zake kalii zilizompa mafanikio na umaarufu ladies free, bongo fleva, dhahabu, hi na nyinginezo ambazo zilimpa mafanikio.
BLUE
Ifahamike Mr. Blue ni miongoni wa wasanii walioanza sanaa ya uimbaji katika umri mdogo, pia ameweza kudumu katika tasnia ya muzikii kwa zaidi ya miaka 10 hadi sasa.
Msanii huyu alipata umaarufu zaidi baada ya kuachia nyimbo kadhaa ikiwemo wimbo wake ulioenda kwa jina la Blue, mapozi na tuko pamoja. Kupitia nyimbo hizo aliweza kuzunguka baadhi ya mikoa ya Tanzania kufanya show katika matamasha mbalimbali.
JUMA NATURE
Aloooh! Muziki wa zamani ulikuwa mtamu asikwambie mtu, kutokana na aina ya utunzi waliokuwa wakitumia ulilenga kufundisha jamii na kuonya.
Baadhi ya ngoma alizoziachia zenye asili kama ya reggae na kuifanya bongo fleva kwa kuelezea maisha ya Watanzania na kuwa hit song ni wimbo wa mtoto Iddi, hakuna kulala, mzee wa busara na inaniuma sana, vilevile Nature ndiye mwanamuziki wa kwanza kwa kipindi hicho kuingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za muziki za MTV Ulaya mwaka 2006.
Katika listi hii ya wasanii waliofanya vizuri katika mUzikii wa bongo fleva, kuna baadhi ya wasanii wameweza kubaki kwenye game toka zamani na wengine kupotea kabisa. Endelea kufatilia jarida letu la Mwananchi Scoop kupata muendelezo wa sababu zilizofanya wasanii hao kupotea kwenye kiwanda cha bongo fleva.
Leave a Reply