Wasanii wa Nigeria Wanavyobebana

Wasanii wa Nigeria Wanavyobebana

Hivi karibuni msanii Teni kutokea Nigeria amekuwa na wakati mzuri kwenye muziki wake baada ya kuachia ngoma ya Money ambayo imeendelea kukimbiza kwenye mitandao ya kijamii lakini pia majukwaa ya kusikilizia muziki.

Stori ni kwamba juzi msanii wa Afrobeat Davido alimwalika Teni kwenye studio huko California ambapo Teni alipata wasaa wa kukutana na Chris Brown kwa mara ya kwanza.

Si hivyo tu, ilimbidi Davido aucheze wimbo wa Teni ‘Money’ ili Chris Brown ausikilize na atoe maksi zake na vyanzo vya karibu tayari vinasema Chris Brown anafikiria kuchapa verse kwenye remix ya wimbo huo.

Kumbuka, hii sio mara ya kwanza kwa Davido kuonesha upendo kwa msanii huyo mwaka 2021 alimpa Teni wimbo mkubwa zaidi katika maisha yake ya muziki ambao unaenda kama 'For You' ambao waliimba pamoja na bado anaendelea kuonesha upendo wake.

Kwa Davido na Breezy wana historia ya kukutana kwenye ngoma kibao za pamoja ambazo zimekuwa na matokeo makubwa ulimwenguni ambapo wamefanya ngoma kama 'Blow My Mind' 2019, 'Sensational' 2023, 'Hmmm' 2024 na nyingine nyingi kwahiyo ni vema pia akiwatafutia wasanii wengine tokea Nigeria nafasi kwa msanii huyo.

Davido anafanya yote hayo akiwa yupo mbioni kuachia album yake ya tano kutoka studio aliyoipachika jina la '5ive' inayotarajiwa kuachiwa April 18, 2025, ikiwa imeshiba majina mazito ya wasanii akiwemo Chriss Brown, Yg Marley, Odumodublvck, Chike, Teni na wengine wengi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags