Wapiganaji 49 wa Al Shabaab wauawa

Wapiganaji 49 wa Al Shabaab wauawa

Serikali ya Somalia imesema wapiganaji 49 wa kundi la Al Shabaab wameuliwa katika operesheni ya kijeshi kwenye eneo la Lower Shabelle kufuatia kampeni inayoendelea kwa miezi kadhaa kwa lengo la kulidhibiti eneo linaloshikiliwa kwa muda mrefu na wapiganaji wa Al Shabab.

Kundi hilo lenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al Qaeda linadhibiti maeneo mengi ya nchi ya Somalia na limedai kuhusika na mashambulio ya mabomu ya mwezi uliopita yaliyosababisha vifo vya takriban watu 120 katika mji mkuu wa Mogadishu.

Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre amesema katika taarifa yake kwamba vikosi vya serikali, vinavyoungwa mkono na wazee wa koo na wanajeshi wa Umoja wa Afrika, wamepata mafanikio katika vita dhidi ya Al Shabaab katika miezi mitatu iliyopita.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags