Wanamuziki waendeshwa na umbea

Wanamuziki waendeshwa na umbea

Wanamuziki wenyewe wanaendeshwa na umbea. Hawaumizi tena vichwa vyao, wanachofanya ni kupita kwenye maeneo yale yale ya umbea.

Matokeo yake Hamisa anatajwa hata mara tatu katika kila wimbo mpya ndani ya mwezi mmoja. Kwa sababu wanafuata mashabiki wanachotaka ubuyu.


Muziki unapotezwa na kiki nyingi za wasanii. Wasanii wetu wengi hapa Bongo, wamekuwa wakitumia kiki kwa ajili ya kutangaza kazi zao. Hili ni jambo baya sana ambalo linaua muziki taratibu.


Kiki zenyewe ni zile zile ambazo zinachosha masikioni. Muziki upo mahala pazuri lakini kiki zinaushusha. Mbosso anaweza kuwa na wimbo mkali lakini kwa kuwa Diamond ana kiki zile zinazobamba atasikika yeye zaidi. Kipaji cha Mbosso kinauawa kwa kukosa kiki za kizinzi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags