Wanafunzi walazwa baada ya kula keki zenye bangi

Wanafunzi walazwa baada ya kula keki zenye bangi

Wanafunzi wasiopungua 90 wa shule ya msingi Soshanguve iliyopo South Africa, wamelazwa hospitali baada ya kula ‘keki’ zinazodaiwa kuchanganywa na bangi.

Kwa mujibu wa Punch news wanaeleza kuwa wanafunzi hao wanaokadiriwa kuwa na miaka 6 hadi 14, walinunua ‘keki’ hizo kwa mfanyabiashara mtaani wakati wakielekea shuleni.

Walimu walipiga simu kwa ajili ya msaada baada ya wanafunzi hao kuonyesha tabia za ajabu na kupatwa na dalili za kuumwa tumbo, kichefuchefu na kutapika.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Elimu ya Gauteng, Matome Chiloane amewataka wazazi kuwa watulivu maana tukio hilo linafanyiwa uchunguzi, pia wazazi kuwaasa watoto kuwa waangalifu kwa vitu wanavyonunua






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags