Waliofariki katika Titan

Waliofariki katika Titan

Waokoaji wamekuwa wakikimbizana na muda kuitafuta manowari ya kitalii iliyopotea siku ya Jumapili karibu na kisiwa cha Newfoundland, Canada katika bahari ya Atlantiki.

Chombo hicho kilizama ili kuyafikia mabaki ya meli ya Titanic, iliyo umbali wa mita 3,800 katika sakafu ya bahari.

Kuzamia hadi katika mabaki hayo kwenda na kurudi inachukua jumla la masaa nane, Lakini timu nyambizi ya Titan inayomilikiwa na kampuni ya Ocean Gate, ilipoteza mawasiliano na meli ya MV Polar Prince, saa moja na dakika 45 baada ya kuzamia baharini, kwa mujibu wa vikosi vya ulinzi wa baharini vya Marekani.

Kikosi cha Marekani na kile cha Canada, wamejaribu kuitafuta manowari hiyo bila mafanikio, hata hivyo jana wamefanikiwa kupata sehemu ya mabaki ya nje ya chombo jicho kilichokuwa kimebeba watu watano ambao ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Gate Stockton Rush (61), wafanyabiashara Hamish Harding (58) pamoja Shahzada Dawood (48) ambaye aliambatana na mtoto wake Suleman (19).

OceanGate hutoza dola za kimarekani 250,000 kwa mtu mmoja kwa safari ya siku nane kuondokea Canada kwenda kutalii mabaki ya Titanic.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags