Timu ya wanasheria wa Diddy inaonekana kuelemewa na kesi za shirikisho huku mmoja wa mawakili wake wa utetezi amepanga kujiondoa haraka katika kesi hizo.
Kulingana na ‘The New York Post’, Anthony Ricco, mmoja wa mawakili sita wanaomtetea Mogul huyo wa hip-hop katika kesi yake ya shirikisho ya usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya biashara za kingono amewasilisha rasmi ombi mahakamani la kujiondoa mapema iwezekanavyo.
Aidha Ricco hakutoa maelezo ya kina kuhusu sababu za kuondoka ghafla, lakini ameeleza kuwa kubaki katika kesi hiyo sio chaguo lake sahihi.
“Kwa hali yoyote ile siwezi kuendelea kumwakilisha Sean Combs kwa ufanisi, Kwa heshima lakini kwa majuto,” aliandika katika hati yake ya mahakama ya shirikisho huko Manhattan.
Utakumbuka Sean "Diddy" Combs anakabiliwa na mashtaka kadhaa katika mahakama ya shirikisho nchini Marekani. Mwezi Septemba 2024, alishtakiwa kwa makosa yanayohusiana na ulanguzi wa ngono kwa nguvu, usafirishaji kwa ajili ya ukahaba, na kula njama za ulaghai.

Leave a Reply