Wakazi ataja vigezo vya msanii bora, aukataa umalkia wa Zuchu

Wakazi ataja vigezo vya msanii bora, aukataa umalkia wa Zuchu

Mwanamuziki wa Hip-Hop hapa nchini, Webiro Wassira 'Wakazi' amedai kuwa ubora wa wasanii duniani kote hutambuliwa kwa vigezo vinavyofanana huku akigoma msanii Zuchu kupewa taji la Malkia wa Bongo Fleva.

Wakazi ameeleza kuwa haijalishi msanii anatoka taifa gani, ukubwa wake utapimwa kwa vitu vinavyofanana kama vile idadi ya ngoma zilizotamba, albamu, idadi ya mashabiki, tuzo, umahiri wake jukwaani na vinginevyo.

Maelezo hayo ya Wakazi yamekuja baada ya mmoja wa mashabiki wake kudai kuwa ubora wa msanii hupimwa kulingana na sehemu aliyopo.

Akipinga hilo, Wakazi ambaye alitoa fursa kwa mashabiki wake kumuuliza maswali na kuyajibu kupitia akaundi yake ya Mtandao wa X (zamani Twitter), ameeleza kwamba: "Popote pale duniani, big, great, legacy artists wana-'common characteristics' uhusika unaofanana, wana hits, wana albums, wana fanbase kubwa, wana impact jamii beyond the music, wana tuzo, wana umahiri wa jukwaani, wana Classic projects, wana skills.

"Haijalishi ni Beyonce, Jay-Z, Wizkid, Miriam Makeba, Diamond Platnumz, Shakira, Angelique Kidjo, Bon Jovi, Usher, Rolling Stones, Adele, Lady Jaydee, Burna Boy, Bob Marley, Bad Bunny, Spice Girls, David Guetta, Hansons, Enrique Iglesias, Carlos Santana, Kidum, Chameleon, AKA, Salif Keita, Joss Stone, Ali Kiba au Shaggy."

Wakati huohuo, Wakazi amegoma mwanamuziki Zuchu kuitwa Malkia wa Bongo Fleva akidai kwamba msanii huyo bado hajafikia vigezo vya kubeba taji hilo.

Wakazi alijibu swali na shabiki yake mmoja aliyetaka kufahamu kama Zuchu anafaa kupewa heshima ya kuitwa Malkia wa Bongo Fleva ambapo amesema: "Anafanya poa sana hits, following, visibility, haipingiki. Ila taji hulibebi tu kirahisi ikiwa unavyofanya wengine wanafanya pia."






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post