Waigizaji wawili maarufu nchini Iran wakamatwa kwa kupinga kuvaa hijab

Waigizaji wawili maarufu nchini Iran wakamatwa kwa kupinga kuvaa hijab

Waigizaji wawili mashuhuri wa Iran wamekamatwa kwa kuunga mkono hadharani maandamano makubwa ya kuipinga serikali, vyombo vya habari vya serikali ya nchi hiyo vimeripoti.

Hengameh Ghaziani na Katayoun Riahi wote wawili hapo awali walionekana hadharani bila hijabu zao - ishara ya mshikamano na waandamanaji.

Maandamano hayo yalizuka mwezi Septemba baada ya kifo cha mwanamke aliyekuwa chini ya ulinzi wa polisi.

Mahsa Amini, 22, alizuiliwa na polisi wa maadili katika mji mkuu, Tehran, kwa madai ya kuvunja sheria kali za hijab. Alikufa mnamo Septemba 16, siku tatu baadaye.

Kulikuwa na ripoti kwamba maafisa walimpiga kwa fimbo na kugonga kichwa chake kwenye gari, lakini polisi walikanusha kuhusiana na swala hilo.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post