Wahukumiwa kwa kutungua Ndege

Wahukumiwa kwa kutungua Ndege

Mahakama nchini Uholanzi Novemba 11, 2022 iliwatia hatiani wanaume watatu bila kuwepo mahakamani kwa mauaji ya halaiki kwa jukumu lao katika kuangusha ndege ya shirika la ndege la Malaysia MH17.

Ndege hiyo ilianguka mashariki mwa Ukraine mwaka 2014 na kuua abiria wote 298 na wafanyakazi waliokuwa ndani ya ndege hiyo.

Wanaume hao watatu, Warassia wawili na mmoja wa Ukraine, walihukumiwa kifungo cha maisha jela.

Kwa sasa wana aminika wapo Russia au wanapigana sambamba na majeshi ya Russia baada ya kuivamia Ukraine.

Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilikuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur ilipotunguliwa Julai 17, 2014, katika miezi ya mwanzo ya vita kati ya waasi wanaoungwa mkono na Russia na wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Donbas mashariki mwa Ukraine.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post