Wachezaji 15 wa timu ya taifa ya wanawake Uhispania wajiuzulu

Wachezaji 15 wa timu ya taifa ya wanawake Uhispania wajiuzulu

Duuuuh! Katika viunga vya michezo nako ni balaa tupu ambapo wachezaji 15 wa timu ya taifa ya wanawake ya Uhispania wamejiuzulu wiki chache baada ya minon'gono ya kuwepo kwa mgawanyiko kwenye kambi ya timu hiyo.

Vyombo vya habari vya Uhispania vimeripoti kwamba baadhi ya wachezaji wa timu hiyo wanataka kocha Jorge Vilda kuondolewa.

Shirikisho la Soka la Uhispania, RFEF limechapisha taarifa jana jioni likisema wachezaji hao 15 waliwatumia barua pepe zinazofanana wakisema wanajiuzulu wakidai mazingira yaliyopo yanawaathiri na yasipobadilishwa hawataichezea timu hiyo.

Hata hivyo shirikisho hilo limesema litawatumia tu wachezaji walio tayari kukitumikia kikosi hicho. Ambapo imeelezwa kuwa hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea kwenye historia ya soka ya Uhispania na ulimwenguni kwa ujumla.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags